Vagabond Multilingual Journal Spring 2014 | Page 10
MCHUMBA HARAMU
(Mtangazaji wa habari kwa jina Neema anawahoji wachumba wawili wanaopendana)
Neema :
Hamjambo
Abdul :
Hatujambo
Neema :
Habari gani
Abdul na Rukia :
Nzuri sana Habari gani ?
Neema :
Nzuri sana. Nyinyi wawili mlikutana namna gani ?
Abdul :
Sokoni
Rukia :
Sote tulikuwa hapo tukinunua machungwa. Tukafikia chungwa moja.
Na hapo tukafahamu kuwa penzi mara moja
Neema :
Sawa. Je mipango ya arusi iko vipi ?
Abdul :
Hatuwezi kusonga mbele bila heri ya wazazi wetu na wao hawatakubali
uhusiano wetu kwa sababu tunaoka makabila tofauti
Neema :
Kuna shida hapo. Tunaweza kuwasikiliza wazazi wenu ?
(mwanahabari anapiga makofi na makofi mengine yanatoka kwenye
hadhira. Wanaingia wanaume wawili na wake zao wawili kwenye
jukwaa wakibishana)
Mke wa 1 :
wewe ni mjinga Mume wa 1 hapana
Mke wa 1 :
hapana wewe mjinga
Mume wa 1 :
(Akielekea walikoketi Abdul na mchumba wake Rukia.) Abdul habari
gani
Mke wa 1 :
(Mke anamsukuma mumewe kado asimsalimu Abdul) Nyamaza
Rukia :
(Akimtahadharisha mamake aache kuleta aibu) Mama
Neema :
Nafahamu kwamba mama na baba Rukia mnatokea kabila la Bukusu
na Mama na baba Abdul mnatokea kabila la Taita sivyo ?
Kuna shida gani hali ikiwa hivyo ?
Baba Abdul :
Mwana wetu anahitaji kuoa mtu wa kabila letu, ni utamaduni.
Mama Abdul :
Kuna wasichana wazuri wengi ambo ni wataita
Mama Rukia :
Binti yangu ni mzuri sana unajaribu kusema nini ?
Baba Rukia :
Mpenzi hakumaanisha…..
Mama Rukia :
Nyamaza mimi ninashughulika haya. (Akimrudia Abdul) Na wewe
huwezi kumwoa binti yangu
Rukia :
Lakini mama tunapendana
Abdul :
Nitatunza binti yako vizuri
Mama Abdul :
Hapana, huyu binti hakustahili wewe Abdul
Baba Abdul :
(Akielekeza swali kwa mwanahabari) Kabila lako gani Wewe ni kabila
la Taita sio ?
10