man maish
focus things
V
ipi wasanii. Siwezi complain. Life
haijanipeleka mbaya after nduthi yangu
kupimpiwa. Wira nimechapa poa na
mfuko haikai mbaya. Heshima yangu ya mtaani
imerudi form.
Sasa Thursday flani niko tu maroundi
mwenda mtaa, then nikaska phone ikilia.
Kucheki ni manzi flani wa mtaa ambaye ni client
loyal. Hadi wa leo sijui ni juju gani nilimwachia.
Na ni manzi kitu hadi mtaa watu humwita tortoise.
Wadhii base huniambia nirushe lugha hapo, lakini hizo
mapressure sipendi. Mimi mtu wa nduthi nitaanzia wapi?
Sasa mimi huyo kuelekea kwake. Nikampata akitegea hapo nje kwa
gate kama amebebea makaratasi kama thao. Kumchapia ananishow
amechelewa auditions.
Yeye hudunga wax kwa kampuni ya talent search. Hizo karatasi
zilikuwa ni CV za wasanii… alikuwa anafaa kuwa amefika by 9
ngware. Kucheki mtambo ilikuwa already 9.15. Lakini uzuri ni hakuwa
anaishia far.
Akanidunga morali vile huwa ameniamini na nitamfikisha in the
shorest time possible. Mistari kama hizo huwa zinanichangamsha
nia je! Nikaseti nduthi vipoa, akadandia, makaratasi ameishikia mbele.
Vile nilikuwa nimemcheki alikuwa ha jamaliza kujipanga. Alikuwa
bado katika harakai za kuchambua hizo karatasi. Nikamshtua akae
chonjo coz airforce iko karibu kupepea.
Akanishow ako chonjo tuelekee, lakini sikuskia ni kama
amenikamata vipoa. Lakini yeye ni kusema, mimi ni kutenda. Ndo
hao sisi teke teke. Kenye napendea Thursday ni vile huwa hakuna
jam mwenda kama ya Monday na Tuesday. So tulikuwa teketeke bila
pressure. Bado njiani, kidogo kidogo huyo tortoise ashaanza njaro
zake za kuchambua karatasi zake.
Nikapinduka kumshow aache kuwa mtricky akuwe mpole
tufike kwanza. Nikiwa katika hizo harakati za kupinduka,
kumbe mbele kuna mlevi anasakata rumba barabarani…
wasee kwa barabara kelele wakinishtua nicheki mbele.
Kupinduka nacheki mdhii zimemamba kwa barabara. Lakini
mi ni yule msee. Nikachapa 1-2 nikamtoka. Hata kabla nijidai,
naskia manduru nyuma yangu.. Ala! Kupinduka naoma
makaratasi zikipeperuka kila pahali. Kumbe huyo manzi
alikuwa ameshtuka akaziachilia. Sasa palikuwa pananyesha
makaratasi.
Noma ilikuwa karatasi zingine zilimwai jamaa wa nduthi
alikuwa nyuma yetu. Sema mdhii kulose control. Sema nduthi
kwa kibanda ya mama mboga. Sema mathe kufunikwa na
mamboga. Sema jamaa wa nduthi kujipata kwa gunia ya
viazi. Noooma sana. Nyuma yangu pia kuna manzi na kelele
zake za kupoteza CV za wasanii na kulia vile atachujwa wax.
Hiyo sasa ilikuwa kelele ya vuvuzela kwangu.
Ameniacha kwa blanda noma na analia vile karatasi
zimepepea. Nilikuwa nimejama a je naye. Tuliachana kama
tumekatziana, hata siko sure kama atawai panda nduthi
yangu tena…
Ilinibidi nimeskizana na msee wa nduthi ili hii story isiende
mbele. Alikuwa msee mpoa. Hata tumekuwa mabeshte. Mathe
naye ilibidi nimelipia mali iliharibika na kumwachia za macho
akanyagie hiyo story. Hata nikipitanga hapo tunagoteana na
huyo matha vipoa.
Mafans, nduthi inaweza kuwa dangerous as much as iko
convenient. Focus ni muhimu sana. Kama wee ni abiria focus
yako inafaa kuwa kwa safety. Biashara zingine malizia mbele
baada ya kufika salama. Tabia ya kubonga na phone, kukata
kucha, kusoma vitabu tusare! Pia pilot ni jukumu lako kumake
sure abiria wako anafollow safety rules vipoa. Tuicheze safe
manze!
16
September 2017